Cristiano Ronaldo amefunga moja ya
magoli mazuri katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa staili ya tik taka na
kuisaidia Real Madrid kuichakaza Juventus kwa magoli 3-0 katika
mchezo wa kwanza wa robo fainali.
Katika mchezo huo ambao Ronaldo
alifunga magoli mawili lakini lilikuwa goli la tiki taka ambalo
halitosahaulika na liliwakuna hata wapinzani wao Juventus ambapo
mashabiki wa timu hiyo walimpongeza.
Ronaldo pia aliweka rekodi ya kuwa
mchezaji wa kwanza kufunga magoli 10 mfululizo katika michezo ya Ligi
ya Mabingwa Ulaya, katika mchezo huo ambao ulishuhudia Paulo Dybala
akipewa kadi nyekundu katika dakika ya 66.
Cristiano Ronaldo akifunga goli la kihistoria kwa staili ya tiki taka na kuwashangaza wengi
Mshambuliaji wa Juventus Paula Dybala akishika kiuno baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu.
Beki Marcelo akifunga goli la tatu la Real Madrid katika dakika ya 74 na kukamilisha ushindi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni