Franck Ribery ameisaidia Bayern
Munich kutokea nyuma na kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya
Sevilla katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya.
Bayern ilipata magoli yake kupitia
goli la kujifunga la Jesus Navas akibambatiza krosi ya Ribery na
kisha kuongeza goli la pili kupitia kwa Thiago Alcantara.
Katika mchezo huo Sevilla ilianza
vizuri na kupata goli la kuongoza katika dakika ya 32 kupitia kwa
beki Pablo Sarabia.
Krosi ya Franck Ribery ikiwa imetinga wavuni baada ya Jesus Navas kujifunga wakati akijaribu kuokoa mpira
Thiago Alcantara akiwa amepiga mpira wa kichwa uliobadilisha muelekeo na kumshinda kipa wa Sevilla
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni