Na Woinde Shizza, Monduli
Zaidi ya wananchi 470 tarafa ya mto wa mbu wilayani monduli mkoani Arusha wamepatiwa huduma ya upimaji wa magonjwa yanayoambukiza na Yale yasioambukiza bure ili kuwawezesha wananchi hao kutambua afya zao
Huduma hiyo ambayo inatolewa na madaktari kutoka Katika chuo cha kijeshi cha monduli (TMA) inatarajiwa kuwafikia wananchi waliopo Katika kata ,Tarafa na vijiji vyote vya wilaya ya Monduli.
Akizungumzia zoezi hilo Katika viwanja vya mto wa mbu ofisa wa TMA ambaye ni nesi Prisca Mwandaji alisema kuwa wao Kama madaktari kutoka chuo cha kijeshi cha monduli (TMA) wameamua kutoa huduma hii ya upimaji WA magojwa yasioambukiza na yale yanayoambukiza hususa ni upimaji wa ugonjwa wa kifua kikuu Pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi(HIV)ili kuwasaidia wananchi wa monduli Kujua afya zao.
"hii ni moja ya kazi zetu wanajeshi kusaidia wananchi hivyo basi Susi kama madkatari tumeamua kujitoleakupima wananchi bure hawachangii hata kidogo na huduma hii tunaitoa katika tarafa zote za wilaya ya monduli na magonjwa ambayo tunapima na kushuri wananchi wanaokuja hapa kupima ni HIV Pamoja na kifua kikuu maana haya nimgonjwa mabaya na yanayoambukiza hivyo ndio maana tunawasisi tiza wananchi wapime ili wajue afya zao ukiangalia na huduma tunatoa bure"alisema Mwandaji
Aidha alisema Kuwa hadi sasa walishapima tarafa Moja ambayo ni makuyuni ambapo jumla ya wananchi 350 na pia hapa mto wa mbu tumeshapima wananchi 470 na bado wanaendelea kuwapima.
"kwakweli kwa upande WA muitikio ni mkubwa maana kwanza hadi sasa kwa hapa mto wa mbu tulishapita malengo tulitarajia kupima watu 450ila tumeshapita adi sasa tumeshapima watu 470 na tunaendelea hivyo kwakweli muitikio ni mkubwa mno kiukweli "alisema Mwandaji
Aidha alimalizia kwakutoa wito kwa wananchi kuwa na desturi ya kupima Mara kwa Mara ilikujua afya zao zipoje kwani iwapo atapima na kujikuta mgonjwa ni vizuri maana ataanza kupata tiba na dawa mapema kabla ya tatizo kuwa kubwa akitolea mfano ugonjwa wa kifua kikuu ambao unaambukizwa kwa njia ya hewa, alimalizia kwakutaja kauli mbiu yao ya ugonjwa wa kifua kikuu kuwa ni"tuwe mstari wa mbele kupambanua na kutatua maambukizi ya kifua kikuu.
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu halmashauri ya wilaya ya monduli Sakina Msangi alisema kuwa nimuimu kupima afya Pamoja na kupata elimu ya afya ilikujua maisha yetu yanaendeleaje kiafya
Aidha alisema kuwa kwa sasa ivi wilaya ya monduli maambukizi ya virusi vya ukimwi yamepungua kwa kiasi kikubwa huku akitoa takwimu kuwa mwaka 2016-2017 kulikuwa na asilimia 6% ya walioambukizwa lakini kwa mwaka 2017 kuanzia January adi December imepungua na kufika asilimia 4% ndio waliopata maambukizi ya virusi vya ukimwi hivyo imepungua kwa asilimia 2%.
Aliwapongeza chuo cha kijeshi cha TMA kwa jinsi walivyoamua kutoa huduma Hizi za upimaji bure kwa wananchi wao kwani wameonyesha kuwa ni kwajinsi gani wao kama watumishi wa serikali wanawajali wananchi wao kwa kuwapima bure na kuwapa elimu ya upimaji afya zao na kutambua faida za kupima afya zao mara kwa Mara na hasara za kutokupima afya zao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni