Utawala wa kifalme wa Abathembu
umesema unaandaa taratibu za maziko ya mwanaharakati wa kupinga
ubaguzi enzi za utawala makaburu nchini Afrika Kusini Winnie
Madikizela-Mandela katika eneo la Qunu huko Eastern Cape.
Wakati utawala huo ukitangaza
maandalizi hayo Rais wa Afrika Kusini Bw. Cyril Ramaphosa amesema
kuwa marehemu, Winnie ambaye anatambulika kwa wengi kama Mama wa
Taifa atafanyiwa maziko ya kitaifa tarehe 14 mwezi huu.
Kufanyika kwa maziko ya Mama Winnie
Mandela Qunu kunatokana na yeye kuolewa mtu wa kutoka ukoo ya kabila
la Abathembu ambaye ni rais wa kwanza mwafrika nchini Afrika Kusini
hayati Nelson Mandela kwa miaka 38.
Msemaji wa ufalme wa Abathembu,
Prince Siganeko Dalindyebo amesema kuwa familia ya kifalme inaona
inaowajibu na kutaka mwili wa Winnie uletwe nyumbani Qunu ambapo
atapumzika kwa amani, kwani kwa mujibu wa mila hakuwa amepewa talaka.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni