Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez amesema anataka kuondoka klabu hiyo na kujiunga na klabu inayoshiriki Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Mchezaji huyo raia wa Uruguay amenuia
kuwasilisha ombi la kutaka kuondoka Liverpool mwishoni mwa wiki iwapo
atanyimwa kuhama.
Suarez ameyaambia magazeti ya Guardian
na Telegraph kuwa Liverpool ilimuahidi ataondoka katika msimu huu wa
joto iwapo klabu hiyo haitafuzu kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni