Uwanja Mkuu wa Ndege wa Kenya wa Jomo
Kenyatta umefungwa kufuatia moto ambao umeteketeza kabisa kitengo cha
wanaowasili cha uwanja huu leo alfajiri.
Moto huo uliotokea majira ya saa 11
alfajiri bado unaendelea kudhibitiwa na vikosi mbalimbali vya zima
moto, huku uwanja huo ukizingirwa na kikosi cha polisi cha (GSU).
Rais Uhuru Kenyatta alitembelea uwanja
huo leo majira saa 3 asubuhi, kujionea hali halisi, vilevile Waziri
wa Mambo ya Ndani Joseph ole Lenk, Waziri wa Uchukuzi Michael Kamau pamoja
na Waziri Anne Waiguru walifika katika eneo la tukio.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni