Alfredo akifurahia matunda ya uvumbuzi wake
Umewahi kufikiria kuwa chupa za maji
zinaweza kutumika kama taa na kuleta mwanga kwenye jengo lenye giza
wakati wa mchana.
Jibu la swali hili analo Alfredo Moser
raia wa Brazili ambaye amebuni taa za chupa za maji ambazo zimepata
umaarufu mno kutokana na kuweza kuleta mwanga ndani ya nyumba bila ya
kuhitaji kutumia umeme.
Taa hizi za chupa za maji, Alfredo
amezibuni kwa kutumia maji yaliyowekwa dawa ya kuondoa madoa (Bleach)
na huning'inizwa katika matundu ya bati ambapo jua likiwaka hupenyeza
mwanga ndani sawa na balbu ya watt 40 hadi 60 kulingana na nguvu ya
mwanga wa jua.
Muonekano wa taa za chupa kwa sehemu ya juu ya bati la nyumba


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni