Polisi wakiutoa dukani mwili wa Beatrice Adhiambo
Watu wenye silaha wamemuua
bibi harusi mtarajiwa kwa kumpiga risasi jana akiwa kwenye duka
aliloenda kununua pete ya harusi kwenye jengo la
Corner katika wilaya ya Kati ya Biashara Jijini Nairobi, nchini
Kenya.
Bibi harusi huyo mtarajiwa
Beatrice Adhiambo Nyaoke, ambaye ni mama wa watoto wanne aliuwawa
ndani ya duka baada ya kupigwa risasi ambapo shemeji yake wa kiume
alijeruhiwa kichwani.
Mumewe Newton Nyaoke
alifanikiwa kunusurika bila jeraha lolote katika tukio hilo
lililotokea jana majira ya saa kumi jioni, na kubadilisha mipango ya
harusi kugeuka kuwa msiba.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni