Jamaa mmoja alikuwa amejipumzisha maeneo ya Coco Beach huku anawaza anayoyajua yeye.
Baada ya dakika 10 akapita mzungu mmoja mbele yake na kumuuliza jamaa " Are you relaxing"
Jamaa hakumuelewa yule mzungu hivyo akaona jibu ni kumwambia " No". Baada ya yule mzungu kuondoka, baada ya dakika nyingine tano akapita mzungu mwingine, alipomuona yule jamaa akawa anampita huku anamuuliza " Are you relaxing".
Jamaa kwa hasira akasimama kisha akamwambia yule mzungu kwa ukali " No"
Alipoona anasumbuliwa sana, akaamua kuondoka eneo lile kwa lengo la kutafuta sehemu nyingine tulivu zaidi ili asisumbuliwe.
Akiwa ametembea umbali kidogo akamuona mzungu mmoja amejipumzisha huku anajisomea gazeti, akamfuata na kumuuliza " Are you relaxing?
Yule mzungu huku kaachia tabasamu pana akamjibu " Yes "
Kwa hasira jamaa akamkwida shati yule mzungu kisha akamchapa makofi mawili ya haraka haraka halafu akamwambia " Kumbe wewe ndio Relaxing eeeh!!, wenzako wanakutafuta kila sehemu wewe umekuja kukaa huku halafu wananisumbua mimi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni