.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Agosti 2013

JAJI NCHINI MAREKANI AZUIA MTOTO KUITWA JINA LA MESSIAH


                                                           Mtoto Messiah DeShwan Martin

Jaji mmoja huko Tennessee nchini Marekani amewaagiza wazazi wa mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi saba kubadili jina lake la Messiah na kuwa Martin, kufuatia mgogoro wa kiimani uliotokana na jina la Messiah.

Katika uamuzi wake huo Jaji Lu Ann Ballew ameeleza kuwa ni mtu mmoja tu anayestahiki kuitwa Messiah naye ni Yesu Kristo.

Hata hivyo uamuzi huo wa Jaji Ballew umeonekana kutomfurahisha mama mzazi Jaleesa Martin ambaye anasisitiza mtoto wake aitwe Messiah DeShwan Martin, na ameahidi kukata rufaa kwenye mahakama ya ngazi ya juu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni