![]() |
| SHEIKH PONDA ISSA PONDA |
Jeshi la polisi mkoani Morogoro limeendelea kukanusha juu ya taarifa zilizoenea kila pembe ya nchi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda kuwa amepigwa risasi na kujeruhiwa na jeshi hilo.
Akiongea na Rweyunga Blog asubuhi hii, kamanda wa polisi mkoani Morogoro Faustine Shilogile amesema mpaka leo hawana taarifa zozote juu ya uvumi huo, na kuwaasa wananchi kutoamini maneno hayo.
Kamanda Shilogile amesema ni kweli jana walipanga kumkamata Sheikh Ponda alipopanda jukwaani kuhutubia katika kongamano lililofanyika mjini humo, lakini hawakufanikiwa kumkamata baada ya kutoroshwa na wafuasi wake.
Amesema katika purukushani za kumkamata, polisi walipiga risasi za baridi hewani ambazo hazina madhara kwa binaadamu ili kujilinda. Hata hivyo amethibitisha kukamatwa kwa watu wawili ambao wanahojiwa na jeshi hilo na kusisitiza kutoa taarifa zaidi baadae.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni