Jumanne, 13 Agosti 2013
PUNGUZA UCHOVU, TABASAMU KIDOGO!!
Utafiti uliofanyika hivi karibuni umebaini kwamba, namba yako ya simu ya mkononi ina uhusiano mkubwa sana na tabia yako.
Yaani asilimia kubwa ya wenye namba za simu zinazoishia na namba zifuatazo wana tabia hizi:-
0 - wenye namba inayoishia na sifuri, huwa ni wakorofi sana nani wabishi sana kila jambo yeye atalipinga hata kama anajua anachokipinga si kweli.
1 - wenye namba inayoishia na moja, hawa wana huruma
sana,ukiwaomba salio wanakurushia mara moja na kama huamini mwambie jamaa yako mwenye namba inayoishia na moja uone kama hajakupunguzi salio.
2 - wenye namba inayoishia na mbili, ni wasikivu sana, ila hawatabiriki muda wowote anaweza kuanzisha ugomvi.
3 - wenye namba inayoishia na tatu, huwa ni wagumu sana kuchangia hasa harusi, lakini kwa kuulizia kila mara maandalizi ya harusi yanaendeleaje hawajambo.
4 - wenye namba inayoishia na nne, huwa ni waaminifu mpaka kupitiliza, yaani huaga hata kwa nyumba nyumba ndogo kuwa wanarudi nyumbani na kweli hapitii kwingine.
5 - wenye namba inayoishia na tano, wanapenda sana kupanda boda boda, wagumu sana kwa hela zao.
6 - wenye namba inayoishia na sita, wanapenda sana kuimba imba, kama huamini angalia namba ya rafiki,ndugu, mume au mkeo kama inaishia na sita utakubali tu mmojawapo ni mwanakwaya.
7 - wenye namba inayoishia na saba, kwa kuomba lifti hawana mfano.
8 - wenye namba inayoishia na nane, kwa kupenda kwenda kwa watu bila taarifa hawajambo
9 - wenye namba inayoishia na tisa, wana aibu sana awe mwanaume au mwanamke.
Haya namba yako inaishia na tarakimu ipi kati ya hizi? Tchao.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni