Jumatano, 14 Agosti 2013
TABASAMU KIDOGO JUAMATANO YA LEO!!
Traffic mmoja aliyekuwa tayari kapiga kinywaji na kalewa mchana kweupe, jana alilisimamisha gari moja dogo lililokuwa linaendeshwa na mwanamama mmoja wa makamo hivi.
Yule mama baada ya kusimamishwa, akaliegesha gari pembeni akimsubiria yule traffic afike amwambie makosa yake. Alipochungulia kupitia kioo cha pembeni, akamuona yule Traffic akimfuata huku akiyumba kutokana na kuzidiwa na kilevi.
Alipofika huku ananuka pombe, yule Traffic akamwambia yule mama amuonyeshe leseni ya udereva. Yule mama akafungua pochi yake, akatoa kioo kidogo cha kujiangalia wakati anajiremba na kumpa yule Traffic.
Alipokipokea, askari yule wa usalama barabarani akakiangalia kile kioo kwa dakika tano huku kakitolea macho kweli kweli kisha akamrudishia yule mama huku anamwambia:-
" Sasa si ungeniambia na wewe ni traffic mwenzangu, haya nenda ila punguza kuchomekea watakugonga afande"
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni