Mzee mmoja maarufu kwa kuogelea, jana saa nane mchana alikuwa anaogelea katika mto Ruvu kwa mbwembwe huku watu mbalimbali wakimuangalia na kumshangilia sana kwa jinsi alivyokuwa anaogelea kwa maarifa makubwa.
Akiwa anaendelea kuogelea huku anaongeza na manjonjo mbalimbali, mara akatokea kibo konyuma yake bila ya yeye kujua.
Basi watu wakaanza kupaza sauti kubwa huku wanamwambia:-
" wee mzee kibokoo!! we mzee kibokooo"
Yule mzee kusikia vile akazidisha sifa akijua wanamuambia yeye ni kiboko kwa kuogelea.
Unajua nini kilimpata? Hapa ndio tupo msibani, karibu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni