.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 12 Oktoba 2013

ICC YATAKA KESI YA ALIYEKUWA MSHIRIKA WA KARIBU WA GADAFFI, SENUSSI IFANYIKE NCHINI LIBYA

Senussi akiwa na Gadaffi wakati huo.

Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC, imeamua kuwa aliyekuwa mkuu wa ujasusi wakati wa utawala wa marehemu Muamar Gadaffi, Abdullah al-Senussi, afunguliwe mashtaka nchini Libya.

Uamuzi huu una maana kuwa ICC haitaendelea kumtaka tena Bwana Senussi kwenda Hague kwa kesi dhidi yake.

Senussi aliyekuwa mkuu wa ujasusi alipatikana na mahakama ya ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu , makosa aliyoyafanywa wakati wa mapinduzi ya kiraia dhidi ya Gaddafi.

Bwana Senussi alikabidhiwa na Mauritania kwa Libya baada ya kukamatwa nchini humo mwaka jana.

Mahakama ya ICC kawaida haiendeshi kesi dhidi ya mshukiwa ikiwa kuna dalili kwamba watatendewa haki nchini mwao.

Aidha katika taarifa yake mahakama hiyo imesema kuwa uamuzi huo hauna uhusiano wowote na kesi dhidi ya mwanawe marehemu Gaddafi,Saif al-Islam 
 Gaddafi anayetakikana na mahakama hiyo.

Islam pia alishtakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita na alishitakiwa pamoja na watu wengine 36.

Saif Gaddafi anazuiliwa na kundi la wapiganaji wa kiisilamu mjini Zintan. 

Mwezi uliopita wapiganaji hao, walikataa kumkabidhi Seif kwa serikali ili aweze kufikishwa mahakamani pamoja na Senussi .

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni