Ushindi wa Super Eagles ya Nigeria ugenini dhidi ya Ethiopia umeipa matumaini ya kushiriki kombe la dunia mwakani.
Ethiopia ilipata goli la kuongoza kunako dakika ya 56 kupitia mchezaji Asefa.
Bao hilo halikukaa kwa muda mrefu, kwani kunako dakika ya 67 mkwaju wa penati uliopigwa na Emanuel Emeni wa Nigeria ulifanya matokeo kuwa 1-1.
Ethiopia watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kutumia nafasi kadhaa walizopata na pengine waliponea chupuchupu kunako dakika 77 ambapo mkwaju wa Nigeria ulirudishwa na mlingoti wa lango.
Goli la ushindi la Nigeria limepatikana kwenye dakika ya mwisho kwa njia ya penalty iliyofungwa kimiani na Emmanuel Emenike na kupalilia njia kwa mabingwa hao wa Afrika ya kwenda Brazil.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni