Naibu Waziri wa Wizara ya Walemavu
nchini Afrika Kusini amesema serikali ya nchi hiyo inachunguza ni
namna gani mtu aliyekuwa akitafsiri kwa ishara wakati wa Ibada ya
Kitaifa ya Kumbukumbu ya Mandela alivyoruhusiwa na maafisa usalama
kuingia kufanyakazi hiyo.
Mtu huyo Thamsanqa Jantjie, ambaye
alisimama pembeni ya viongozi wa dunia katika Ibada hiyo amekanusha
kuwa ni tapeli na kusema alichanganyikiwa alipoona malaika wakija
katika uwanja na kuanza kupatwa na mawenge.
Taasisi ya Wakalimani wa Lugha za
Ishara zinazotumika kwa watu wenye tatizo la kusikia imesema
imeshapeleka mara nyingi malalamiko kuhusiana na utendaji kazi mbovu
wa Jantjie kwa chama cha ANC, hakijachukua hatua yoyote.
Baada ya kuibuka malalamiko kwa watu
wanaotambua lugha ya ishara kuwa mtu huyo alichokuwa anakifanya ni
upuuzi na hakikuwa na maana yeyote, ofisi ya wakala iliomuajiri
kufanya kazi hiyo nayo imetoweka.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni