Sanamu kubwa zaidi duniani ya Nelson Mandela
imezinduliwa katika mji mkuu wa Afrika kusini Pretoria siku moja baada
ya rais huyo wa zamani kuzikwa.
Sanamu hiyo iliyotengenezwa kwa shaba ina urefu wa mita tisa na ina uzani wa tani nne nusu. Ilizinduliwa katika bustani la majengo ya bunge na inaonyesha Nelson Mandela akihimiza umoja na maridhiano.
Sanamu hiyo yenye mikono ya Mandela ikiwa wazi ilinuiwa kuonyesha Mandela alivyoliungaisha taifa zima kwa mapenzi yake.
Familia ya Madiba , viongozi wa ANC , viongozi wa Afrika na maafisa wengine wakuu walihudhuria mazishi ya Mandela yaliyofanyika katika kijiji cha Qunu mkoani Cape Mashariki juzi jumapili.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni