Ratiba ya hatua ya 16 bora michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya imetolewa ambapo inaonyesha kuwa timu ya soka ya Manchester City ya Uingereza inaanza hatua hiyo ya 16 bora kwa kupambana na Barcelona ya Uhispania, wakati Manchester United yenyewe inaingia katika kibarua cha kupambana na Olympiakos.
Matajiri wa London Chelsea chao kibarua ni dhidi ya Galatasaray ili hali Arsenal itakuwa mwenyeji wa Bayern Munich toka Ujerumani.
Ac Milan wao watakuwa nyumbani kuwaalika Atletico Madrid, wakati wao Bayer Leverkusen watakuwa wenyeji wa Paris St Germain. Wenyewe Real Madrid wanaingia hatua hiyo kusafiri kuwafuata Schalke.
Zenit St Petersburg wao watakuwa nyumbani kuwaalika Borrusia Dortmund. Mechi za kwanza zitachezwa kati ya tarehe 18/19 na 25/26 mwezi wa pili mwakani na marudio ni kati ya tarehe 11/12 na 18/19 mwezi wa tatu mwakani





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni