Wagonjwa hapo jana
wametimuliwa kwenye hospitali za umma mashariki mwa Kenya, kufuatia
mgomo wa watumishi wa afya unaoendelea.
Ndugu za wagonjwa
walikusanyika kwenye vituo vya afya kuchukua wagonjwa wao wakati
mgomo wa watumishi wa umma ukiingia siku ya saba.
Katika hospitali
ya rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga iliyopo Kisumu kunataarifa kuwa
wagonjwa waliondolewa kwa nguvu kutoka vitandani na walinzi wa
hospitali hiyo.
Hospitali ya
wilaya ya Kisumu imefungwa lakini wagonjwa ambao hawana ndugu
kuwasaidia kuweza kutoka wamebakia katika hospitali hiyo
iliyotelekezwa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni