Hospitali ya Taifa ya Kenyatta nchini
Kenya imesema watoto wachanga wanane wamekufa kabla ya mama zao
kujifungua kutokana na ukosefu wa huduma za afya kutoka na mgomo wa
madaktari unaoendelea.
Aidha kitengo cha watoto njiti pamoja
na wale wenye matatizo mbalimbali katika hospitali hiyo kimezidiwa na
watoto kutokana na watoto kutolewa kwenye hospitali hiyo kutokana na
kukosekana kwa huduma kwenye hospitali zingine za umma.
Kutokana na hali hiyo kitengo hicho
chenye uwezo wa kulaza watoto 40 katika vizimba vya kukuzia watoto
njiti, kina watoto 122 hali inayofanya watoto watatu hadi watano
kuchangia kizimba kimoja, kinachopaswa kulaza mtoto mmoja.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni