.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 18 Desemba 2013

WATU WAPATAO 500 WADAIWA KUFA KATIKA MAPIGANO SUDAN KUSINI

Mamia ya watu inaaminika wamekufa kwenye mapambano nchini Sudan Kusini yanayohusisha majeshi ya serikali na kundi lililojitenga.

Wanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa wameambiwa na vyanzo mbalimbali vya habari katika Mji Mkuu wa Juba kuwa vifo vinaweza kuwa kati ya watu 400 hadi 500.

Sudan Kusini imekuwa kwenye siku mbili za machafuko, kufuatia taarifa ya kutokea jaribio la mapinduzi dhidi ya Rais Salva Kiir.

Taarifa za awali zilisema maafisa 10 wa ngazi za juu serikalini, akiwemo Waziri wa Fedha wamekamatwa kwa kuhusishwa na jaribio hilo la kupindua serikali.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni