Hali ya Usalama
katika Jamhuri ya Afrika ya Kati imezidi kuwa mbaya licha ya
kuapishwa kwa rais wa muda wa nchi hiyo.
Mkuu wa Shirika la
Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa
wananchi waislam sasa wapo katika hali ya hatari mno.
Taarifa yake
imekuja wakati ambapo Viongozi wa Waislam na Wakristo wakikutana na
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kuomba msaada zaidi wa
Kimataifa.
Karibu watu
milioni moja sawa na asilimia 20 ya wananchi, wamekimbia makazi yao
baada ya kuibuka vurugu za kidini katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni