Mkuu
wa wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a akizungumza na maafisa ugani wa
Halmashauri ya wilaya ya Kalambo alipofungua kikao kazi chao cha siku
mbili jana katika kijiji cha Msanzi kata ya Msanzi wilayani humo
NA RAMADHANI JUMA,KALAMBO
Zaidi ya Maafisa kilimo 40 wa wilaya ya Kalambo wanakutana kwa muda wa siku mbili katika kikao kazi kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati ya kuinua uzalishaji na kuwainua wakulima wa wilaya hiyo ili waondokane na hali ya umasikini.
Kikao kazi hicho kinachofanyika
katika kijiji cha Msanzi wilayani humo ni sehemu ya utekelezaji wa
Mpango wa serikali wa “Matokeo Makubwa Sasa” katika sekta ya kilimo.
Akifungua kikao kazi hicho,
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a aliwataka Maafisa hao kuwa mfano
wa kuigwa na wakulima wa wilaya hiyo kwa kuwa na mashamba yao
yaliyolimwa kisasa.
Aliwataka pia kuhakikisha kila
kata na vijiji wanakofanyia kazi kunakuwa na shamba darasa lenye ukubwa
usiopungua robo eka kwa ajili kutolea mafunzo kwa wakulima, sambamba na
utunzaji wa takwimu halisi kwa vpindi tofauti ili kuwa utendaji kazi
wenye tija na unaopimika.
Aliwaagiza pia kusimamia kwa
karibu utekelezaji wa kila shule ya msingi na sekondari wilayni kulima
shamba lisilopungua ekari tano ili wanafunzi wapate uhakika wa chakula
wakati wa masomo kwa lengo la kuinua kiwango cha ufaulu.
Mwishoni mwa mwaka jana, mkuu
huyo wa wilaya alitangaza mpango wa kuzipatia shule zote wilayani humo
vocha tano za pembejeo ili zifanikishe uzalishaji wa chakula cha
wanafunzi wanapokuwa masomoni
Wilaya ya Kalambo yenye Kata 17 na Vijiji 100 ina maafisa kilimo zaidi ya 40 waliopo katika kata na vijiji hivyo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni