Watu wengi hasa wazazi wamemshambulia mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa nchini Marekani Beyonce Knowles kutokana na kivazi chake alichokuwa amevaa wakati akitumbuiza wakati wa utoaji wa tuzo Grammy Awards zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita huko Marekani.
Akiwa anatumbuiza jukwaani huku akipigwa tafu na mumewe ambaye naye ni mwanamuziki mahiri Jay Z, Beyonce alivaa nguo ambayo inaonyesha sehemu kubwa ya mwili wake.
Hali hiyo iliwafanya mashabiki wake hasa wazazi kutoa maoni yao mbalimbali kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter wakihoji kama kweli Beyonce ni mzazi, na mtoto huyo na watoto wengine waliokuwa wakifuatilia tukio hilo kubwa lililoonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni watajifunza nini toka kwake kutokana na kuvaa hivyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni