Bunge la Ukraine limepiga kura na kuifutilia mbali sheria iliyokuwa na utata ya kuzuia maandamano, sheria ambayo imeleta wimbi kubwa la machafuko nchini humo.
Kura hiyo imepigwa huku Waziri Mkuu wa Ukraine, Mykola Azarov ( pichani juu ) akitangaza kujiuzulu wadhifa wake huo katika jitahada za kujaribu kumaliza maandamano yaliyoikumba miji mbalimbali ya nchi hiyo



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni