Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika
Kusini,(Democratic Alliance) kimemtangaza Dr Mamphela Ramphele ambaye
pia alikuwa mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi kuwa mgombea wake wa
uchaguzi mkuu mwezi Aprili.
Bi Ramphele, aliyekuwa mwandanani wa mpigania uhuru Steve Biko, aliunda chama chake cha kisiasa cha Agang mwaka jana.
Kiongozi wa chama cha Democratic Alliance, Helen Zille alisema hakuna mwanasiasa mwingine mwenye uwezo wa kutawala nchi hiyo kama Bi Ramphele.
Wadadisi wanasema kuwa hatua hii inalenga kuondoa tuhuma kuwa chama cha DA kina ufuasi mkubwa wa waafrika wazungu na kwamba hakiwezi kupata ushindi kwa hilo.
Viongozi hao wawili walisema kuwa kuungana kwao kutaleta umoja miongoni mwa wananchi Afrika Kusini , umoja ambao marehemu Mandela alipigania.
Bi Ramphele, mwenye umri wa miaka 66, anaonekana kama mtu mwenye ajenda nzuri na pia anasifika kwa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi baadhi ya mambo ambayo yanawashawishi watu kupiga kura.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni