Januari 27 raia
mwingine wa China Tang Yong Jian alifikishwa mahakamani, Kenya baada ya
kukutwa na Kilo 3.4 za pembe za ndovu akisafirisha kwenda Guangzho,
China akitokea Msumbiji.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Raia wa China
Chunsheng Zhang amekamatwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Jomo Kenyatta JKIA Jijini Nairobi nchini Kenya akiwa na pembe za
ndovu.
Mtuhumiwa huyo
alikamatwa katika uwanja huo akitokea Lubumbashi Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC), akiunganisha ndege
kuelekea Guangzhou
nchini China.
Zhang ambaye
alikuwa abiria katika ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways
alikamatwa jana usiku akiwa na bangili, mikufu iliyotengenezwa kwa
pembe za ndovu na vipande kumi vya pembe za ndovu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni