Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni UNESCO limeonya kwamba kiwango duni cha Elimu
kinachotolewa kinajenga ongezeko kubwa la watu wasiojua kusoma kuliko
inavyodhaniwa.
Ripoti mpya iliyotolewa na shirikisho
hilo la UNESCO inaonyesha kuwa takribani watu milioni 175 katika nchi
masikini, robo ya idadi hiyo ikiwa ni
vijana hawawezi kuandika au kusoma
sentensi moja iliyokamilika.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa katika nchi
nyingi za Kusini mwa Sahara idadi ya watoto kati ya wainne hadi
watano kutoka katika familia masikini
wanamaliza elimu ya msingi bila
kujifunza kanuni za awali za kusoma na kuhesabu.
Shirika la UNESCO limesema dola bilioni
130 hupotezwa kwa kutumika visivyo kila mwaka kutokana na elimu
duni.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni