Chama Tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF
kinapanga kuchangisha dola milioni moja kwa ajili ya sherehe ya
kuadhimisha siku ya kuzaliwa rais Robert Mugabe ambaye atatimiza umri
wa miaka 90 mwezi ujao.
Katibu wa Masuala ya Vijana wa chama
cha Zanu-PF Absalom Sikhosana amekaririwa na mtandao wa
newzimbabwe.com kuwa maandalizi kwa ajili ya shuhguli hiyo maalumu
yanaendelea vizuri.
Rais Mugabe ataadhimisha siku ya
kuzaliwa Februari 21 lakini sherehe zimepangwa kufanyika Februari 23
huko Marondera.
Kiongozi huyo aliyezaliwa mwaka 1924,
ameitawala nchi hiyo tangu mwaka 1980 na ni kiongozi mzee zaidi
kuliko wote barani Afrika.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni