Mwezi mmoja baada ya kujeruhiwa katika ajali ya
mchezo wa kuteleza kwenye barafu, meneja wa bingwa wa mashindano ya mbio
za magari ya langalanga, Mjerumani Michael Schumacher amesema
kwamba madaktari wanaendelea kumwangalia kwa karibu kwani hali yake kiafya bado haijatengemaa.
Bingwa huyo mara saba aligonga kichwa chake katika mwamba wakati akiteleza kwenye barafu katika milima ya Alps
nchini Ufaransa.Madaktari wanatumia madawa kumpa usingizi wakijaribu kupunguza uvimbe na kuchubuka kwenye ubongo wake.
Tayari wamemfanyia upasuaji mara mbili kuondoa damu iliyoganda kwenye ubongo.
Hata hivyo huenda maisha yake yakawa hatarini iwamo ataendelea kuwa katika hali ya kuzirai kutokana na hatari ya ubongo wake kuharibika na kupata maambukizi ya kifua.
Mashabiki wa Michael Schumacher wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa nje ya hosipitali alikolazwa



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni