Waendesha mashtaka
nchini Misri wamesema waandishi 20 wanakabiliwa na mashtaka nchini
humo.
Kumi na sita
miongoni mwao ni raia wa Misri wanaotuhumiwa kuhusika na kundi la
kigaidi na wanne ni raia wa kigeni wanaotuhumiwa kulisaidia ama
kusambaza habari za uongo za kundi hilo.
Watuhumiwa hao ni
pamoja na Waingereza wawili, Mholanzi mmoja na raia wa Australia
mmoja ambaye anaaminika kuwa ni mwandishi wa kujitegemea wa
al-Jazeera, Peter Greste.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni