Bwana Ramesh
yupo nchini kuangalia mazingira ya Kampuni yake kutaka kujenga chuo cha ufundi
Zanzibar kitakacholenga kutoa mafunzo ya ufundi ndani ya eneo la Mashariki na
Kusini mwa Bara la Afrika.
Kushoto ya
Balozi Seif ni Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Mh. Ramadhan Abdulla
Shaaban na kulia yake ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Alu
Juma Shamhuna pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mh. Moha Aboud Mohd.
Kati kati
yao ni Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Zanzibar Mh. Ramadhan Abdulla
Shaaban.
Kushoto ya
Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF
} Nd. Abdullwakil Haji Jecha mkutako uliofanyika nje ya Makazi ya Balozi Seif
Bara bara ya Farahani Mjini Dodoma.
Picha na
Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } unaendelea na utafiti wa namna ya kutaka
kuliimarisha eneo la kati la Mji wa Zanzibar ili liwe katika hadhi
inayokubalika Kimipango Miji sambamba na kuleta haiba nzuri ya Mji.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko huo Nd. Abdullwakil Haji Jecha alisema hayo wakati
akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo nje
ya makazi yake Bara bara ya Farahani Mjini Dodoma.
Nd.
Abdullwakil alisema Uongozi wa Mfuko huo umefikia uamuzi huo kufuatia hatua
nzuri iliyofikiwa ya ujenzi wa Kiwanja cha Kufurahishia Watoto cha Uhuru –ZSSF
kilichopo kariakoo na Mnara wa kumbu kumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar
miradi iliyo chini ya ujenzi wa Mfuko huo.
Alieleza
kuwa uimarishaji wa eneo hilo umelenga kujenga bara bara zitakazokwenda sambamba na uwekaji wa
mapembea ya kuchezea watoto baina ya miradi hiyo miwili jirani.
“ Sisi tuko
tayari na tumejiandaa kutumia wataalamu na washauri washirika katika
kuliimarisha eneo hilo kwa ujenzi wa mapembea Maduka ya Kisasa kulingana na
ushauri wa Taasisi inayosimamia mipango miji “. Alisisitiza Nd. Abdullwakil.
Akizungumzia
ujenzi wa nyumba za mkopo zilizoko katika ramani ya ujenzi zinazotaka kujengwa
na Mfuko huo katika eneo la Mbweni Ndugu Abdullwakil Haji Jecha alisema hatua
za micho za michoro ya nyumba hizo imeshakamilika.
Aliiomba
Serikali Kuu kusaidia upatikanaji wa eneo maalum la uwekaji wa karakana ya
utengenezaji wa Matofali pamoja na vifaa vyengine vya ujenzi litakalotumiwa na Kampuni iliyokubali kuingia
ubia na Mfuko huo ya Shumaka ya Nchini Marekani katiika ujenzi wa nyumba hizo.
Naye Waziri
wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Zanzibar Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban ambae
alikuwepo kwenye mazungumzo hayo aliuahidi Uongozi wa Mfuko huo kuupatia eneo
la Buyu kwa ajili ya kuwekea kara kana yao.
Waziri
Shaaban alisema eneo hilo lilikuwa likitumiwa na Kampuni ya ujenzi ya
Engineering construction ambayo tayari imeshakamilisha mkataba wake hapa
Nchini.
Akitoa
Shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliuagiza
Uongozi huo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } kuwasiliana na
mshirika wao wa ujenzi wa nyumba hizo za mkopo ili hatua za mradi zianze mara
moja.
Balozi Seif
aliutoa mashaka Uongozi wa Mfuko huo kwamba wateja wa ununuzi wa nyumba hizo
wapo wengi hasa ikizingatiwa kwamba Zanzibar hivi sasa inaendelea kubadilika
Kiuchumi na kibiashara Kiamataifa.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Mfuko huo kwa jitihada zake
inazochukuwa za kuanzisha miradi tofauti
yenye lengo la kutunisha mfuko huo kwa faida na hatma njema ya wanachama wake.
Wakati huo
huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa
mazungumzo na Uongozi wa Kampuni inayojihusisha na utoaji wa mafunzo ya Ufundi
{ European Erum } kutoka London Uingereza.
Katika
mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi ya muda ya Balozi Seif iliyopo ndani ya jengo la Msekwa
Bungeni Dodoma Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Europea Erum Bwana Ramesh Kumar
alisema Taasisi yao imeonyesha nia ya kutaka kujenga chuo cha ufundi Zanzibar.
Bwana Ramesh
ambae Kampuni yake tayari inefungua Matawi yake Ghana na Siera Leon Afrika
Magharibi alisema Uongozi wa Kampuni hiyo umekusudia kuweka Tawi lake Zanzibar
ili kutoa huduma za Taaluma ya Kiufundi ndani ya Mataifa ya Mashariki na Kusini
mwa Afrika.
Alifahamisha
kwamba mradi huo utakaojumuisha Majengo la vifaa vyake Kamili umelenga
kutumia jumla ya Dola za Kimarekani
Milioni tano ambazo ni kama mkopo utakaorejesheka kutokana na ada za wanafunzi
watakaojiunga na chuo hicho.
Mkurugenzi
huyo wa European Erum alisisitiza kwamba taaluma itakayotolewa na Kampuni hiyo
ambapo wanafunzi wahusika waliomaliza Darama la Kumi na Mbili na Kumi na Nne
itamuwezesha mshiriki wa mafunzo hayo ya miaka mitatu kuweza kujitegemea katika
soko la ajira katika fani ya ufundi.
Naye kwa
upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliuomba
Uongozi wa Kampuni hiyo hiyo kuandika maombi maalum ya uanzishwaji wa mradi huo
wa uwekezaji utakaosaidia kwa kiasi kikubwa suala la ajira kwa vijana
watakaomaliza mafunzo yao.
Balozi Seif
aliuhakikishia Uongozi wa Kampuni hiyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
itatoa kila msaada katika kuona mradi huo unafanikiwa kuanzishwa hapa Nchini.
Mapema
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Ali Juma Shamhuna aliushauri Uongozi
huo kukifanyia utafiti chuo cha Ufundi Mbweni kama majengo yake yanaweza kufaa
kwa kuandishwa mradi huo.
Waziri
Shamuhuna alisema taaluma inayotolewa na Kampuni hiyo imeonyesha kulingana na
mafunzo yanayotolewa na Chuo cha Ufundi Mbweni. Hivyo utafiti huo unaweza
kusadiai kupunguza gharama ya ujenzi wa majengo mengine kwa ajili ya chuo
hicho.
Othman
Khamis Ame
Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
25/2/2014.




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni