| Gari la Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe likipita kwa shida katika barabara ya Rupingu -Ludewa jana |
| Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akkitazama sehemu ya barabara ya Rupingu – Ludewa inayoporomoka kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha |
| Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akionyesha madhara ya Mvua yaliyopelekea barabara ya Rupingu -Ludewa kuharibika |
Na Francis Godwin,Blog
MVUA
kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeno mbali mbali ya hapa
nchini zimeendelea kuleta madhara makubwa katika wilaya ya Ludewa
mkoani Njombe baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe
kukesha akifungua barabara na wananchi wake baada ya kukwama
kuendelea na ziara ya kuwatembelea wapiga kura wake wa kata ya
Rupingu kutokana na kifusi na miti mkuporomoka na kuziba barabara
hiyo ya Ludewa – Rupingu .
Tukio
hilo lilitokea juzi majira ya saa 3 asubuhi wakati msafara wa
mbunge huyo wenye magari matatu kujikuta ukikwama katika eneo la
Mlima Rupingu kwenye barabara ya Ludewa- Rupingu umbali wa Kilomita 15
hivi kutoka mjini Ludewa hali iliyomlazimu mbunge huyo na viongozi
mbali mbali wa CCM wilaya ya Ludewa kuungana na wananchi waliokuwa
wakielekea kuzika kufanya kazi ya kuzibua barabara hiyo.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi wananchi wa Rupingu ambao walikuwa
wamekwama katika eneo hilo kwa zaidi ya siku tatu na maiti yao
iliyokuwa ikisafirishwa kwenda kijijini walisema kuwa mvua hizo
zimeendelea kuleta madhara makubwa katika barabara hiyo na kuwa wao
wamepata kukwama eneo hilo kwa zaidi ya siku tatu kutokana na
maporomoko ya kifusi katika barabara hiyo.
Alisema
John Haule kuwa uwezekano wa wao kukamwa kwenda kuzika ulikuwa
mkubwa zaidi kama mbunge wao asingekuwa katika ziara kuelekea
Rupingu kwani kufanya ziara kipindi hiki cha masika kummemfanya mbunge
kujua kero hiyo.
“Kwanza
tunampongeza sana mbunge wetu Filikunjombe wabunge waliopita
kipindi kama hiki cha mvua walikuwa hawafiki vijijini zaidi ya
kuishia Ludewa mjini ila yeye anafanya ziara wakati wote na kuona
changamoto mbali mbali ambazo wananchi wake tumekuwa tukizipata ….
hivi ni kiongozi gani anakubali kushuka katika gari lake na kuingia
katika tope kuchimba kifusi pamoja na wananchi wake….kweli Ludewa
tumempata mbunge wa wananchi kweli sio mbunge wa kujitumikia yeye na
familia yake”
Hata
hivyo alisema barabara hiyo ambayo ipo chini ya wakara wa barabara
mkoa wa Njombe imeendelea kuboreshwa toka alipoingia Filikunjombe
madarakani na mkoa wa Iringa kugawanywa .
Kwa
upande wake mbunge Filikunjombe mbali ya kuwapa pore wafiwa hao
na wananchi wa Rupingu kwa kukosa barabara kutokana na mvua hizo bado
alipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na uongozi wa TANROADS mkoa
wa Njombe katika kuzihudumia barabara hizo kwani alisema ubovu wa
barabara hiyo unatokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kama
ambavyo maeneo mengine yanavyopata madhara kama hayo .
Hivyo
alisema kwa upande wake anapongeza jitihada za TANROADS mkoa wa Njombe
kwa kuendelea kuboresha barabara hiyo ya Rupingu-Ludewa ambapo kwa
mwaka jana imeboresha kwa mamilioni ya shilingi na mwaka huu imetengewa
zaidi ya Tsh milioni 400
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni