Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
amekasirishwa na kitendo cha kurekodiwa kwa siri wakati akiwakosoa
washambuliaji wake.
Mourinho amesema ni aibu mtu kurekodi
mazungumzo binafsi, yaliyorushwa na Televisheni ya moja ya Ufaransa.
Mourinho amesema alikuwa akitania
wakati alipokuwa analalamika kuhusu washambuliaji wa Chelsea ambapo
alirekodiwa akisema anafikiri Samuel Eto'o anaumri wa miaka 35 na
wala si 32.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni