Mahakama nchini Misri imewahukumu
adhabu ya kifo watu 26 kwa kosa la kuanzisha kikundi cha kigaidi kwa
lengo la kushambulia meli zinazopita katika mfereji wa Suez.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya
Misri watu hao pia wametuhumiwa kutengeneza mabomu na milipuko
mingine mbalimbali, ambapo hukumu hiyo imetolewa leo bila wao kuwepo
mahakamani.
Hukumu hiyo imekuja siku moja tu baada
ya Waziri Mkuu mpya mteule Ibrahim Mahlab kuapa kuuvunja ugaidi
katika kona zote za nchi hiyo.
Bw. Mahlab ameteuliwa kuunda serikali
mpya ya nchi hiyo baada kujiuzulu ghafla kwa Waziri Mkuu wa mpito
Hazem Beblawi na baraza lake lote siku ya Jumatatu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni