Marekani imezitaka pande zote kutulia na kujizuia uchochezi,
wakati huu ambapo Ukraine ikiwa kwenye hali ya tahadhari katika mkoa wa Crimea.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry, amesema
ameongea na Urusi ambayo imeahidi kuheshimu mipaka ya Ukraine. Hata hivyo
ameionya Moscow kusimamia kauli yake.
Mapema jana watu wenye silaha wanayoiunga mkono Urusi
walivamia bunge dogo la Crimea, huku urusi ikifanya mazoezi ya kijeshi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni