.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 28 Februari 2014

MAMLAKA YA BANDARI KUANZA KUTOA HUDUMA KWA SAA 24 KUANZIA KESHO



Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ikishirikiana na wadau wake kuanzia kesho wanatarajia kuanza kutoa huduma kwa saa 24, siku saba za wiki, mwaka mzima bila kupumzika.

Ofisa Uhusiano wa TPA, Janeth Zurangi amesema uamuzi huo ambao unakusudia kuongeza ufanisi wa bandari hiyo, umefikiwa baada ya wadau mbalimbali kutia saini mikataba ya utekelezaji kazi hiyo.

Zurangi amesema ingawa kulikuwapo mabishano kuhusu vipengele kadhaa ndani ya mkataba huo, wadau wote walikubali kuanza kutoa huduma kila siku kwa saa 24 kuanzia Machi Mosi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni