Wabunge wa Bunge
la Kenya wanataka kufanya mabadiliko katika muswada wa ndoa ili
kuondoa kifungu kinachoonekana kuwa ni kikwazo kwa wanaume wanaoamini
katika ndoa zamitala.
Kifungu hicho
kinachoonekana kuwa ni kikwazo kwa wanaume ni cha 44 cha muswada huo,
ambacho kinapendekeza chini ya ndoa za kimila mwanaume anapaswa
kuomba ridhaa ya mkewe kabla ya kuongeza mke mwingine.
Muswada huo ambao
umepita katika awamu ya pili hapo jana, pia umeibua mkanganyiko
kuhusiana na iwapo wanawake watakuwa na mamlaka ya kiasi gani ya
dhidi ya uamuzi wa wanaume wao wanaotaka kuongeza wake.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni