.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 28 Februari 2014

SIKINDE YAANZA KUIPUA NYIMBO MPYA

Inline image 1
 Hatimaye bendi kongwe, bendi pekee ambayo imepata kuwa mabingwa wa muziki nchini mara zote mbili ambazo mashindano hayo yamepata kufanyika, bendi ya  Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma ya Ukae” imeanza kuipua nyimbo zake mpya zitakazokuwa katika album mpya ya “Jinamizi la Talaka” itakayozinduliwa mwaka huu 2014.


Album hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo 7. Mpaka sasa Sikinde wameishazitoa nyimbo tatu za 1. Jinamizi la Talaka, 2. Za Mkwezi Mbili na 3. Nikipata Nitalipa.


Nyimbo hizi unaweza kuzisikiliza online au ku-download kwenye mtandao wa https://www.hulkshare.com/sikinde


Nyimbo 4 zilizobakia ambazo nazo zitatolewa muda wowote kuanzia hivi sasa ni 1. Kibogoyo, 2. Dole Gumba, 3. Ng'ombe Haelemewi na Nundu na 4. Tabasamu

Hii ni album ya kwanza kutolewa tokea mwaka 2009 iliporekodiwa album ya “Supu Umeitia Nazi” album iliyomfanya mwimbaji wake Karama Regesu kuchukua zawadi katika Kili Music Award ya mwaka 2009 kwenye category ya “Mtunzi Bora wa Muziki

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni