.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 28 Februari 2014

SIKU CHACHE BAADA YA RAIS MUSEVENI KUIDHINISHA SHERIA YA KUPIGA MARUFUKU USHOGA, BENKI YA DUNIA YASITISHA MSAADA WA DOLA MILIONI 90

Benki ya dunia imesitisha msaada wa dola milioni 90 kwa Uganda ,ikiwa ni siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo kupitisha sheria mpya ya kupiga marufuku mapenzi ya jinsia moja.

Benki hiyo imesema kuwa inataka kufanya tathmini yake kuhakikisha kuwa malengo yake ya maendeleo nchini Uganda katika sekta ya afya, ambayo msaada huo ulikuwa umeelekzwa, hayataathirika .

Sheria iliyoidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Wafadhili wengine tayari wameanza kusitisha misaada Uganda. Wahisani kama Denmark na Norway wamesema kuwa wataanza kufadhili mashirika moja kwa moja badala ya serikali.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni