.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 26 Februari 2014

WANASHERIA KENYA WATISHIA KUSHINIKIZA KUONDOLEWA IGP KIMAIYO

Chama cha Wanasheria nchini Kenya (LSK) leo kimetishia kutaka kuondolewa kwa mkuu wa jeshi la polisi nchini humo IGP David Kimaiyo ikiwa atashindwa kutii amri ya mahakama ya kumkamata Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mutea Iringo.

Mwenyekiti wa LSK Eric Mutua amesema kitendo cha kutokutii amri ya mahakama kilichofanywa na Kimaiyo ni msingi wa kuondolewa madarakani, hatua ambayo LSK itachukua iwapo atashindwa kutekeleza amri halali ya mahakama.

Jaji George Odunga aliamuru Katibu Mkuu Iringo kukamatwa baada ya kushindwa kulipa fidia ya shilingi milioni 31 kwa raia wa Tanzania aliyewekwa kizuizini kimakosa na kuteswa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni