.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 1 Machi 2014

HALMASHAURI YA JIJI : JE HAWA NI SAHIHI KUWEPO KATIKA ENEO HILI?

Hawa nao wanauza Viatu pande hizi kwa bei nafuu...

Hii ndiyo hali Halisi ya eneo kutoka Ubungo Darajani karibia na mitambo ya Gesi hadi eneo la watu wanaopandia magari ya kwenda Mwenge? Je Halmashauri ya Jiji hamlioni hili? Je Manispaa husikia nanyie hamlioni hili? Au hili ni eneo halali limepitishwa kwa ajili yakufanya biashara hizi?
Wengine wanauza samaki katika eneo ambalo kiafya sio sahihi.

Hili ni eneo la Ubungo ambalo limekuwa na wimbi kubwa lawafanya bishara wadogo wadogo kuegesha biashara zao za kila ainapembezoni mwa njia za wapita kwa miguu jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Licha ya usumbufu na kero hiyo, eneo hilo kutokana na msongamano wa watu wengi sana, limekuwa ndio maskani kwa vibaka ambao hujipatia kipato chao bila hata ya jasho kwa kujichanganya humo kama raia wa kawaida na kufanya wizi.

Wakizungumza watumiaji mbalimbali wa barabara hiyo wamelilalamikia Jiji na Manispaa husika kwa kushindwa kuwataftia eneo husika wafanyabiashara hao wadogo wadogo na kwamba kutokana na uzembe huo mkubwa wa kutowazuia naowameamua kuendelea kuleta kero

"Eneo hili kwa kweli linatia Aibu sana kwa sababu hapa ndipo Lango kuu lakuingia jijini na mara watu wanapo ingia wanakutana na kero hii ambayomimi binafsi naita ni uchafu, nasikitika sana kuona Jiji na Halmashari husika wameshindwa kabisa kudhibiti na kuwataftia eneo husika hii ni
aibu"

Alizungumza mmoja wa watumiaji wa barabara hiyo ambaye hupita mara kwa mara. 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni