Timu ya soka ya Bayern Munich ya Ujerumani imefanikiwa kusonga mbele katika ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya robo fainali baada ya kuiondoa Arsenal hapo jana usiku katika mchezo wa marudiano kwa kufungana bao 1-1.
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanjwa wa Allianz Arena, Bayern Munich ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kunako dakika ya 54 ya kipindi cha pili kupitia kwa Bastian Schweinsteiger kabla ya Arsenal kusawazisha dakika ya 57 kupitia kwa Lukas Podolski.
Bayern imesonga mbele kwa tofauti ya mabao 3-1, baada ya kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa awali jijini London
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni