.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 11 Machi 2014

WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA WAPITISHA KANUNI ZA KULIONGOZA BUNGE HILO

Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba akiwaleza jambo wajumbe wa Bunge Hilo kabla ya kuahirishwa mpaka kesho jioni na Kuwataka wale wanaotaka kuchukua fomu ya uenyekiti kuanza kuzichukua leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti wa Kamati ya Uundaji wa Kanuni zitazotumika katika bunge Maalum la Katiba Prof. Costa Ricky Mahalu akisoma azimio la kutunga na kupitisha kanuni za bunge Maalum.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba akiiunga Mkono Azimio la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Dkt. Fransis Michael akiwaomba wajumbe wa bunge maalum la katiba kuunga mkono na Kupitisha Azimio la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba ili kuwa na umoja na kutekeleza jukumu hili la kitaifa leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba na Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Mhagama akiunga Mkono Azimia la Kutunga na Kupitisha kanuni za Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni