Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na Mwenyekiti
wa CCM Iringa Vijijini Mama Delfina Mtavilalu mara baada ya kuwasili
katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa ambapo alipokelewa na baadhi ya
viongozi wa mkoa huo na kuelekea moja kwa moja ofisini ambapo alifanya
mazungumzo mafupi
Akizungumza
na waandishi wa habari huku akionyesha moja ya gazeti lililowahi
kuripoti kampeni hizo kwa picha Philip Mangula amelaani kampeni alizodai
zinadhalilisha watoto zinazofanywa na CHADEMA huku akionyesha mmoja wa
watoto ambaye alipigwa picha huku akionyesha sare zake za shule ambazo
zimechakaa na kuchanika na mmoja wa wapiga debe wa chama hicho akisema
kutangaza umasikini wa mtu ni kumdhalilisha 

Philip
Mangula akiingia katika ofisi za mkoa wa Iringa huku akiwa ameongozana
na Katibu wa Mkoa wa Iringa Bw. Hassan Mtenga na viongozi wengine.
Mwandishi wa habari wa ITV Bw. Silvanus Kigomba akiuliza swali kwa Mzee Philip Mangula wakati wa mkutano huo.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akielezea mambo mbalimbali
yanayohusu uchaguzi huo ambapo amesema CCM ni waumini wa Amani na kwamba
katika jimbo la Kalenga hagombei Godfrey Mgimwa bali kinachogombea ni
Chama cha Mapinduzi kwani ungekuwa ni ukoo wa Mgimwa unagombea basi
ungeona akina Mgimwa woote wako mbelea wakipiga debe ili washinde lakini
kwa sababu ni CCM inagombea ndiyo maana utaona viongozi na wana CCM
mbalimbali wakishiriki katika kampeni hizo ili kukipatia ushindi chama
chao.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni