.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 12 Machi 2014

MAUAJI YA MPENZI WAKE, MAMBO YAZIDI KUMUELEMEA OSCAR PISTORIUS MAHAKAMANI

Kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius imeendelea leo huku mtaalam wa uchuguzi wa uhalifu akitoa maelezo kwa vitendo akionyesha namna mwanariadha huyo alipojaribu kuvunja mlango wa choo kwa gongo la kuchezea Kriketi baada ya kumpiga risasi Reeva Steenkamp.
Polisi Johannes Vermeule mwenye cheo Kanali ameiambia mahakama wakati huo Pistorius hakuwa amevalia miguu yake ya bandia kutokana na urefu wa eneo alilokuwa akijaribu kuvunja mlango kuwa chini kiasi
Ushahidi huo ni muhimu kutokana kukinzana na taarifa za Pistorius kuwa alisogelea mlango wa bafu Februari 14 mwaka jana akiwa amevaa miguu yake bandia wakati alipofyatua risasi chooni akidhani kuwa amevamiwa na mtu na kumua mpenzi wake Reeva
 Ushahidi ukionyeshwa mahakama jinsi Pistorius alvyovunja mlango kabla ya kumfikia mpenzi wake na kumpiga risasi
Oscar Pistorius akiwa mahakama hii leo wakati kesi yake ikiendelea kuunguruma

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni