.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 4 Machi 2014

OSCAR ALIZWA NA UTETEZI WA WAKILI WAKE BAADA YA KUELEZEA RISASI ZILIVYOHARIBU UBONGO WA MPENZI WAKE

Oscar Pistorius ameangua kilio leo mahakamani wakati wakili wake alipokuwa anajenga hoja kuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp alikuwa amedhurika mno ubongo kutokana na risasi alizopigwa, kiasi cha kushindwa kuweza kupiga mayowe kama ilivyodaiwa.

Wakili Barry Roux ametoa madai hayo katika kujibu ushahidi wa jirani wa Pistorius ambaye alidai mahakamani kuwa alisikia marehemu Reeva akipiga mayowe na kisha kusikia risasi katika usiku ambao modo huyo aliuwawa.

Wakili huyo ameiambia mahakama kutatolewa ripoti kuwa madaktari kuonyesha ubongo wa marehemu ulivyoharibika kutokana na risasi, hali ambayo haiwezekani kupiga mayowe. Kauli hiyo ilimfanya mtuhumiwa wa mauaji hayo Oscars kuziba masikio yake kwa mikono na kuangua kilio.




Hakuna maoni :

Chapisha Maoni