.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 6 Machi 2014

TAIFA STARS KUREJEA KESHO JIONI KUTOKA NAMIBIA

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kurejea nchini kesho (Machi 7 mwaka huu) kutoka Windhoek, Namibia kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA.

Taifa Stars ambayo katika mechi hiyo dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ilitoka sare ya bao 1-1 itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.

Timu inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager baada ya kuwasili itakwenda hoteli ya Accomondia kwa ajili ya chakula cha mchana na baadaye kuvunja rasmi kambi yake.

Boniface Wambura Mgoyo

Media and Communications Officer

Tanzania Football Federation (TFF)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni