Mwandishi wa habari, Ndg Francis Dande (wa kwanza kulia) akijaza fomu ya kujiunga na mfuko wa pensheni wa PPF jana mara baada ya mkutano wa waandishi na wadau wa habari kumalizika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar Es Salaam, Mkutano huo uliandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF ulilenga Kuwapa elimu waandishi na wadau wa habari nchini juu ya huduma nyingine zinazotolewa na Mfuko huo wa PPF.
Mwandishi wa Habari wa Kituo Cha Runinga cha ITV, Bi Fatma Almasi Nyangasa akijaza fomu ya kujiunga na mfuko wa Pensheni wa PPF jana mara baada ya mkutano wa waandishi na wadau wa habari kumalizika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar Es Salaam, Mkutano huo uliandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF.
Mdau wa Habari Nchini Bw Albart Jackson (wa Pili Kulia) akijaza fomu ya kujiunga na mfuko wa Pensheni wa PPF jana mara baada ya mkutano wa waandishi na wadau wa habari ulioandaliwa na mfuko wa Pensheni wa PPF kumalizika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari nchini wakijaza fomu ya kujiunga na mfuko wa pensheni wa PPF jana katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar Es Salaam mara baada ya mkutano wa waandishi na wadau wa habari uliondaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kumalizika
Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (wa kwanza kushoto) akiwapa maelekezo waandishi wa habari jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga na mfuko wa Pensheni wa PPF jana Katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar Es Salaam mara baada ya Mkutano wa waandishi na wadau wa habari kumalizika
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni